July 12, 2017


Rooney alijiunga na timu hiyo mwishoni mwa wiki iliopita akitokeaManchester United ambapo amesaini mkataba wa miaka miliwi Everton baada ya kuitumikia Man U kwa miaka 13, amerejea katika timu yake zamani ambayo alichezea tangu akiwa kinda.
Nyota huyo wa timu ya taifa England yupo nchini kwa ziara maalum na timu hiyo ambapo ataonekna uwanjani kwa mara  ya kwanza akiwa na jezi ya Everton kwenye uwanja wa huo wa Taifa kabla ya kurejea England kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya msimu mpya wa EPL na michuano mingine.Rooney anatarajiwa kuwa hamasa kubwa kwenye mchezo huo wa kesjo ambao unasubiliwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini pamoja na Afrika Mashariki kwa ujumla.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV