MASHABIKI WA SIMBA WACHARUKA, KINACHOENDELEA HIVI SASA NI MATUSI KWA WINGI KWENYE AKAUNTI YA BANDA INSTAGRAM
Na George Mganga
Mashabiki wa klabu ya Simba wamemvaa kwa kumshambulia na matusi makali mchezaji anayekipiga Baroka FC ya Afrika Kusini, Abdi Banda, kwenye akaunti yake ya Instagram.
Banda ambaye anatumia jina la 'Officialabdibanda24' Instagram, ametukanwa matusi ya kila aina kufuatia kauli yake juu ya Afisa Habari wa Simba kuwa aliwahi kuitisha kikao na Waandishi wa Habari kulalamikia penati.
Banda ambaye aliwahi kuichezea Simba, alinukuliwa akitamka kauli hiyo wakati akifanyiwa mahojiano na Mwandishi na Mhariri Mkuu wa Gazeti la Championi kupitia Global TV, Saleh Ally.
Kitendo cha kutoa kauli hiyo kimewafanya mashabiki wengi wa Simba kuanza kumshambulia kwa matusi makali baada ya Manara kutangaza kusikitishwa na kauli ya Banda, mapema leo asubuhi.
Wengi wamemtuhumu wakiandika ni mapema mno kutoa kauli kama hiyo kwasababu ndiyo kwanza ameanza safari ya maisha ya soka nje ya Tanzania.
Wapo pia walioandika wakimuonya asijaribu kutoa kauli kama hizo kwa viongozi waliomsaidia kufika hapo alipo na badala yake ajitume na kupambana zaidi ili afike mbali kisoka.
Manara aliandika kupitia Instagram akieleza kushangazwa na kauli ya Banda huku akisema ni wajibu wake kuongelea kila linalojiri ndani ya Simba, sababu ni wajibu wake kufanya hivyo.
Manara povu lanini tena........ Banda Kaongea ukweli
ReplyDeleteHakuna cha povu dogo anajiona yupo juu Mara nyingi akihojiwa anawalaumu wenzie hawamtafuti kwann asiwatafute wenzie timu huko kwani hajui matatizo ya wachezaji wa bongo na viongozi?
ReplyDeleteKisoka bado na akumbuke vyombo vya habari ndio wanawaua soka mfano no Nditi mdogo wa Chelsea yupo wapi Leo? Amekuja hapa wakina Shaffih dauda wamemsifia na dogo akatanuka mabega Leo yupo wapi? Banda hata kwa Samatta hatafikia
Povu tu hakuna cha zaidi mwacheni kijana awe huru kueleza kile anachokiona. Kama kuna kitu simba mnamdai elezeni acheni povu. Huyu kijana ni hazina kubwa kwa Taifa acheni fitina zenu. Banda utafanikiwa kwa msaada wa Mungu. Walikuwa wanataka kukuharibia jinsi walivyomharibia Ndemla na hana hata nafasi kubwa kwenye kikosi.
ReplyDeletekwani swali aliloulizwa lilihusu Simba au kiongozi wa Simba? si aliulizwa kuhusu yeye
DeleteUnaposema ni sahihi una maana ipi? Ebu tuongelee facts juu ya hicho alichosema japo alikuwa OP kwani jibu na swali aliloulizwa havikuendana. Kuna kosa gani la kimaadili au ambalo haliruhusiwi katika soka kwa mdau wa soka au viongozi na wachezaji kulaumu upumbavu wa marefa? Nitajie sheria hata moja inayozuia mtu kulaumu maamuzi mabovu ya marefa? Tuliangali mechi ya Kirafiki kati ya Stars na Benin refa akawapatia penati isiyo stahili wabenn tukafungwa goli ambalo halikupswa, mbona Banda au watanzania wengine hawakusem kwamba tusimlaumu refa kwa sababu kumlaumu ni vibaya na hawezi kupata moyo wa kuchezeha mechi yetu. Mbona tulisema waziwazi kuwa refa katunyonya? Umesikia CAF wanatuadhibu kuwa kumlaumu yule refa ni kosa? Mara nyingi tunapenda kuiga kwa wale tunaodhani kwamba wameendelea kisoka. Mara ngapi wachezaji wa Ulaya katika ligi kubwa pamoja na viongozi na makocha wanalalamikia maamuzi mambovu ya maerfa uwanjani? Mbona hatusemi kwamba ni jambo baya? Ukweli wa Banda hapo uko wapi? Je, yeye huwa halalamiki uwanja kuhusu makosa ya waamuzi? Juzi mechi ya Stars na Congo kafanya faulu za ovyo lakini alionekana akilalamikia uamuzi wa refa wa kumuadhibi. Je, huo sio ulalamikaji? Manara kama kiongozi wa klabu angewezaje kulalamikia uwanjani hali ye si mchezaji? Ni lazima alalamikie katka press conference kwa sababu ndio mahala pake. Alichokifanya Manara ni kuitetea timu yake na kutimiza majukumu ya kazi yake pale anapoona hakutendewa haki na wala si yeye tu duniani kote hata hapa Bongo (hata hao wanaomsifia Banda leo) huwa wanafanya hivyo sema tu kwa kuwa alichokilalamikia Manara kinawagusa maana kilikuwa ni advantage kwa upande wao. Tumeshuhudia mwamuzi wa aliyechezesha mechi ya South Africa na Senegal akiadhibiwa kwa makosa aliyoyafanya ya kuibeba South, wasingelalamika Sengal unadhani FIFA wangefanya maamuzi waliyoyafanya? Hoja ijibiwe kwa hoja na wala si mihemuko, unaposema Banda kasema ukweli, kwanza ujiulize ukweli ni nini na ni ukweli upi aliosema? Je jibu la swali lake linaendana na alichoulizwa? Yeye alipo ni professional hapaswi kuendelea kuwa na ujinga kama ule wa kipindi yuko bongo. UKINIJIBU UJIBU KWA HOJA NA SI MIHEMUKO!
ReplyDeleteTatizo la huyu bwana mdogo Banda anajiona kucheza mpira South Africa ndio babu kubwa.Ingawa South Africa ina nafuu kulinganisha na kwetu Tanzania kulinganisha masilahi lkn kwangu binafsi siukabli kihivyo soka la South Africa na inabidi Banda aachane na maneno bali ajiongoze na siku ya mwisho atimize malengo.Aachane na lawama amabzo zimeshapitwa na wakati na zimebaki historia.
DeleteMwingine anazungumzia kuwa Simba wamembania Ndemla.Simba wanahusika vipi kumbania ilihali amekwenda kufanya majaribio na wamesema alifaulu.Je ofa iliwekwa mezani?Kama iliwekwa mezani ilifanikiwa thamani ya mchezaji kuuzwa?Au ndio yale ya Kapombe unamtoa bure kwa kisingizio cha kupandisha kiwango kwanza na mauzo baadaye kumbe yote ni deals na baadaye unastukia amerudi bongo na kuvaa jezi ya timu nyingine kwa bei ya buree.Kwa hili viongozi wa Simba kuweni makini kwa maana Simba ndio imekuwa inapoteza wachezaji wao kirahisi bila kutarajia na wengi wao wameanzia tokea Simba B.
ReplyDelete