July 19, 2017



Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, raia wa Cameroon, ameuambia uongozi wa timu hiyo kumpeleka nchini Afrika Kusini mshambuliaji, Thomas Agyei baada ya kukoshwa na uwezo wake kufuatia kutazama video zake.

Simba wanamfuatilia Agyei kwa ajili ya kumuongeza ndani ya kikosi chao ambapo hivi karibuni kigogo mmoja wa timu hiyo alimfuata nchini Ghana kwa ajili ya kumalizana naye.

Chanzo kimesema kuwa awali dili hilo lilitaka kukwama baada ya viongozi kutia ngumu kusajiliwa kwake kwani walishindwa kuona video zake akicheza baada ya kigogo huyo aliyekwenda Ghana kushindwa kuzituma video hizo.

“Unajua awali viongozi walitaka kumuacha mshambuliaji huyo baada ya yule aliyetumwa Ghana kushindwa kutuma video kama ambavyo walikuwa wanataka, lakini yeye alifanya hivyo kutotuma kwa makusudi kwani alihofia kusambaa.

“Lakini alipomuonyesha kocha Omog kabla ya kwenda Sauz, yeye alimkubali na kutaka aletwe kambini fasta kwa ajili ya kuungana na wenzake ili amuangalie kwenye siku hizo 20 ambazo tutakaa huko.


“Kocha alikoshwa na uwezo wake (Thomas) kwani kwenye hizo video zinaonyesha akifunga mabao ya hatari ya kichwa na hata miguu yote lakini kubwa zaidi ana spidi ya kuwatoka mabeki,”  kilisema chanzo hicho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic