Timu ya wataalamu wa vipimo ya
Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) kuangalia kama wachezaji wanatumia dawa
zinazozuiwa michezoni, imevamia mazoezi ya Barcelona.
Timu hiyo ambayo haikutoa taarifa
ilivamia mazoezi hayo jana asubuhi na kufanya vipimo kwa baadhi ya wachezaji.
Hakukuwa na taarifa kama wageni hao
kutoka Uefa wangetembelea viwanja vya timu hiyo ingawa imekuwa ni kawaida
wakati wa kuelekea michuano ya Ligi ya Mabingwa.
Wataalamu hao baada ya kufika uwanjani
hapo, walisababisha mazoezi kusimama na wao wakachagua baadhi ya wachezaji si
kwa kufata majina au namba, badala yake waliyemuona wanaweza kumpima.
Waliopimwa ni Pedro, Cesc, Iniesta,
Neymar, Messi, Song, Adriano, Alves, Afellay na Cuenca.
Baada ya kumaliza kazi yao, wataalamu
hao wa Uefa walibeba vifaa vyao na kuondoka, majibu hayajatolewa.
0 COMMENTS:
Post a Comment