Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Chelsea wameanza vibaya msimu mpya baada ya kuchapwa kwa mabao 3-2 wakiwa nyumbani Stamford Bridge jijini London.
Chelsea wamefungwa na Burnley katika mchezo uliotawaliwa na vituko vya kila aina.
Hadi mapumziko Chelsea ilikuwa nyuma kwa mabao 3-0 huku ikiwa imempoteza beki wake Garry Cahill.
Kipindi cha pili Alvaro Morata alijitahidi kufunga bao moja, lakini dakika chache baadaye kiungo mkongwe Cesc Fabregas akalambwa kadi ya pili ya njano na kuzaa nyekundu.
Wakiendelea kucheza pungufu, Chelsea walikupata bao la pili lililofungwa na beki David Luiz na ndiyo ukawa mwisho uliozaa matokeo ya mabao 3-2.
0 COMMENTS:
Post a Comment