August 7, 2017Uongozi wa Yanga, umelazimika kumnunua beki Gadiel Michael kwa shilingi milioni 10 akitokea Azam FC ambapo ameshakabidhiwa nyumba ya kupanga jijini Dar.

Beki huyo amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Azam ambapo wiki iliyopita Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa aliulalamikia uongozi wa Azam kuwatajia dau kubwa licha ya mchezaji huyo kubakisha mkataba mfupi.

Inadaiwa awali Yanga walitakiwa kutoa shilingi milioni 40 kabla ya kupunguziwa na kutakiwa kutoa Sh milioni 20 ambayo bado kwao ilionekana ni nyingi hali iliyosababisha Azam wawaambie Yanga wataje kiasi walichokua nacho, wakamalizana kwa Sh milioni 10.

“Baada ya majadiliano ya muda wakakubaliana kiwango hicho, Yanga wakapeleka, wakakabidhiwa mchezaji na tayari wamempa nyumba Gadiel,” kilisema chanzo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Hussein Nyika, kwa upande wake alisema: “Siwezi kuzungumzia fedha ila ni kweli kwa sasa Gadiel ni mchezaji wetu baada ya kumsajili kwa mkataba wa miaka miwili na tumeshampatia nyumba ya kuishi hapa mjini ili aweze kuifanya kazi  vizuri.”0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV