August 3, 2017



Idara ya Uhamiaji Tanzania, imemaliza utata juu ya uraia wa mgombea wa urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, baada ya kusema ni raia halali wa Tanzania tofauti na wengine wanavyosema.

Uhamiaji wamefikia hatua hiyo baada ya Karia kuwekewa pingamizi na mgombea mwenzake, Imani Madega ambaye alisema mgombea huyo si Mtanzania, bali ni Msomalia, hivyo hana vigezo vya kushiriki Uchaguzi Mkuu wa TFF unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.

Msemaji Mkuu wa Uhamiaji, Mrakibu Ally Mtanda, amesema: “Baada ya kupokea taarifa hiyo, tumefanya uchunguzi na kubaini kwamba Karia ni Mtanzania na wala si Msomalia.


“Karia alizaliwa hapa nchini ambapo mama yake ni Mtanzania wakati baba yake ni Msomalia. Kutokana na msingi huo, Karia ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa chini ya kifungu 5(1) na (2) cha sheria ya uraia ya Tanzania sura ya 357 (Rejeo la 2002 na kanuni zake. 

"Wakati huohuo akiwa raia wa Somalia kwa kurithi. Ni hitaji la kisheria chini ya kifungu cha 7(1), pale mtu anapokuwa  na uraia wa nchi mbili kuukana uraia wa nchi moja anapofikisha umri wa miaka 18 hatua ambayo Karia aliitekeleza na kuthibitishwa ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic