August 3, 2017

Msemaji wa Simba, Haji Manara ameamua kufanya "uchale" baada ya kuiwakilisha Yanga wakati wa hafla fupi ya ukabizishwaji vifaa iliyofanywa na wadhamini wa Ligi Kuu Bara, Vodacom.

Manara alikwenda moja kwa moja jukwaani wakati vijana waliokuwa wakiiwakilisha Yanga kupanda jukwaani kutambulisha jezi hizo.

Kwa kuwa hakukuwa na mwakilishi wa Yanga, Manara alipanda jukwaani na kusema anawawakilisha akifanya utani ingawa baadhi walimpongeza na kusema aliiwakilisha timu ya baba yake, Sunday Manara, naye akasema hawezi kuwa Yanga hadi anakufa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV