August 22, 2017Kuna uwezekano mkubwa Kocha Joseph Omog akamuacha mshambulizi wake, Emmanuel Okwi acheze winga ya kushoto kama ilivyozoeleka.

Simba inavaa Yanga katika mechi ya Ngao ya Jamii, mchezo utakaopigwa jijini Dar es Salaam.

Awali, baada ya Okwi kutua Simba, Omog alionekana kutaka kumjaribu acheze kama namba 10 yaani inside left.

Katika mazoezi ya mwisho ya Simba mjini Unguja, Zanzibar, Okwi alirejea kucheza pembeni kama alivyozoea.

Okwi kucheza kuchoto imekuwa hatari zaidi kwa timu pinzani kwa kuwa mguu wake wa kulia una nguvu zaidi ya kupiga mashuti. Hivyoa napotokea kushoto, anakuwa na nafasi kubwa ya kupiga akiwa karibu na lango.


Tayari kikosi kizima cha Simba, akiwemo Okwi kimetua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi hiyo ya kesho kwenye Uwanja wa Taifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV