August 4, 2017
Kampuni ya King’amuzi ya Startimes Tanzania imeingia kwenye udhamini wa mchezo wa mpira wa kikapu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambapo watadhamini kuanzia mzunguko wa pili hadi utakapomalizika pamoja na gharama zote za uwendeshaji.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Dar es Salaam, Okere Emisu alisema mzunguko wa kwanza walikuwa na changamoto ya viwanja lakini kwa udhamini wa StarTimes wana imani tatizo hilo litatuliwa.

“Kampuni ya StarTimes na Sibuka wameamua kutudhamini kwa kupitia vipindi vyao wataonyesha michuano hii, lakini kama mwanzo nilivyosema kuwa tuna upeleka mchezo huu kibiashara zaidi.

“Mzunguko wa kwanza tulikuwa na changamoto za viwanja vya kuchezea, kwa udhamini huu nafikiri tatizo hilo litatatuliwa," alisema Okere Emisu.


Naye ofisa uhusiano wa kampuni hiyo, Samweli Gisayi alisema udhamini huo utaufikisha mbali mchezo huo na watatumia vipindi vyao kuonyesha kwani wana uhusiano na Shirika la Mpira wa Kikapu la Kimataifa (FIBA). 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV