August 4, 2017Wachezaji wapya wa Yanga wakiongozwa na Ibrahim Ajibu, kiungo Raphael Daud na kipa Mcameroon, Rostand Youthe kwa mara ya kwanza kesho Jumamosi wataitumikia timu hiyo kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Singida United itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar.

Singida United inafundishwa na bosi wa zamani wa Lwandamina, Mholanzi Hans van der Pluijm.

Yanga chini ya kocha wake, George Lwandamina wanaendelea na mazoezi yao ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi mkoani Morogoro ambapo wameweka kambi ya muda mfupi.

Lwandamina raia wa Zambia amesema mchezo huo utakuwa kipimo cha kuangalia wachezaji wake kama wapo tayari kwa ajili ya ligi msimu ujao baada ya kufanya mazoezi ya pamoja kwa muda mrefu.

"Muda mrefu tumekuwa tukifanya mazoezi tu, tulianza gym kule Dar kabla ya kuhamia uwanjani, lakini kwa kipindi hicho chote hatukuwa na kipimo cha kuona wapi tumefikia na kwa namna gani tupo kamili kwa ajili ya msimu ujao.


"Mchezo huu utatuonyesha udhaifu na ubora wetu uko wapi, pia kwa mara ya kwanza nitaona uwezo wa wachezaji wapya na kuanzia hapa ndipo nitajua kama wataingia kwenye kikosi cha kwanza ama la," alisema Lwandamina.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV