August 31, 2017


KAIMU Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Kidao amesema kuwa ameagizwa na rais wa Shrikisho hilo, Wallace Karia kumwandikia barua Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi ili kuwaadhibu viongozi wa Bodi ya Ligi waliohusika na kupanga ratiba.

Kumekuwa na malalamiko kutokana na Bodi hiyo kupanga ratiba ya ligi ambapo walishindwa kuzingatia kuwa kuna michezo ya kimataifa ambayo itahusisha timu za taifa jambo ambalo limesababisha baada tu ya mchezo mmoja tu, ligi hiyo ikapanguliwa tena.

“Nimeagizwa na rais nimwandikie barua mtendaji mkuu wa bodi ya ligi ili aweze kuwachukulia hatua viongozi wa bodi hiyo waliohusika na kupanga ratiba hii pamoja na kwamba walikuwa na kalenda lakini bado wamekosea,” alisema Kidao.


Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi ni Boniface Wambura ambaye sasa atakuwa na jukumu la kuchukua hatua kwa wasaidizi wake.

1 COMMENTS:

  1. Ukurupukaji mwingine!!! Hivi ina maanisha wakati ratiba inaandaliwa na bodi ya ligi Viongozi wa TFF hawakuipitia na kuihakiki ili kuepuka misigano? Nasisitiza viongozi hawa wa sasa ndio walewale wa TFF iliyopita sikutarajia kuona mambo mapya zaidi ya yaleyale yaliyopita. Viongozi hawa wa TFF ni walewale wa toka miaka ya 1990 na wameendelea kuwemo humo wakijirithisha na kurithisha uongozi wa watu wao. Kwa hakika watapatikana wahanga wengi ili wanaoua soka wakiendelea kujihalalishia mambo ambayo si mazuri katika soka letu. Naamini katika weledi na mabadiliko ya kimfumo kuwa ndilo suluhisho sahihi la matatizo tunayokutana nayo.
    Nimewasilisha.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic