August 8, 2017
Beki wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, ameanza kutoa vitisho kwa timu pinzani ikiwemo Simba baada ya kusema kuwa, kikosi chao kwa sasa kipo kamili kwa kupambana na timu yoyote katika Ligi Kuu Bara.

Ninja aliyejiunga na Yanga hivi karibuni akitokea Taifa Jang’ombe, Jumamosi iliyopita alicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Singida United kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-2.

Ninja amesema mechi hiyo imeonyesha ni kwa jinsi gani wapo vizuri na ndiyo maana wameshinda, hivyo wapo tayari kwa kuanza mikikimikiki ya ligi kuu ambapo huko watakutana na Simba ambao ndiyo wapinzani wao wakubwa.

“Kikosi chetu kipo vizuri, ukiangalia mpaka sasa tupo vizuri katika kila idara na tupo tayari kupambana na timu yoyote ile ambayo itakuja mbele yetu, kwa kifupi tumejiandaa vema kuanza ligi.


“Najua kila timu imejipanga vizuri kuhakikisha inafanya vizuri msimu ujao, lakini niwaambie tu, sisi tupo vizuri zaidi, hivyo wajiandae na vichapo,” alisema Ninja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV