September 22, 2017


SIKU chache baada ya kupigwa kiwiko na kupoteza fahamu, kiungo mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Martin, ameibuka na kutamka kuwa mchezaji wa Majimaji aliyempiga kiwiko alidhamiria kumuua.

Hiyo, ikiwa ni siku chache tangu kiungo huyo apate fahamu na kuanza mazoezi ya pamoja na wenzake kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam wakati timu hiyo ikijiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda FC itakayochezwa kesho Jumamosi.

Kiungo huyo alipigwa kiwiko hicho na beki wa Majimaji inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya Sokabet, Juma Selamba na kusababisha ashindwe kuendelea na mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya 1-1.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Martin alisema kikubwa anachoshukuru hivi sasa ni kiwiko hicho hakijampata vizuri, lakini anaamini kama kingempata, basi angepoteza uhai palepale uwanjani.

Martin alisema, beki huyo alikuwa ana nia mbaya ya kumtoa uhai na siyo kitu kingine na hata kiwiko amepigwa kwa makusudi na siyo bahati mbaya kama inavyoelezwa.

"Nikwambie kitu kimoja ambacho watu hawakifahamu, mimi yule beki tunafahamiana vizuri, yeye anakaa Tegeta na mimi ninakaa Kawe.

"Mara kadhaa tumekuwa tukikutana katika timu moja kwenye kazi zake za nje (ndondo) sasa nikashangaa kuona akinifanyia vitu vya kihuni na kishamba.

"Kiukweli kabisa, nilipanga kumrudishia mara tutakapokutana kwenye mechi ya marudiano kwa sababu alikuwa ana nia mbaya ya kutoa uhai wangu kwa makusudi, lakini nimeamua kutomrudishia rafu, sitamsamehe kwa sababu siyo mtu mzuri kwangu kwani alitaka kuniua kwa makusudi," alilalamika Martin.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic