September 1, 2017



Beki mkongwe wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amepewa majukumu mapya ndani ya kikosi hicho ambapo kwa sasa ana uwezo wa kuchagua mechi za kucheza tofauti na hapo awali pamoja na kumshauri kocha.

Cannavaro ambaye amedumu kikosini hapo kwa takriban miaka 12 sasa, amesema majukumu aliyonayo sasa, yanamfanya asionekane sana uwanjani akicheza.

Beki huyo ambaye pia ni nahodha, hajaonekana akiwa na jezi za Yanga katika mechi mbili zilizopita ambazo timu hiyo imecheza ikiwemo ile ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba na ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli.

 Cannavaro amesema kuwa, kwa sasa hatarajii kuonekana sana uwanjani kutokana na jukumu alilonalo la kutoa ushauri kwa Kocha George Lwandamina na wachezaji wenzake ambapo anahitaji kutoa nafasi zaidi kwa vijana ili watumikie taifa.

“Ni kweli kwa sasa sichezi sana kwani mimi nina muda mdogo wa kucheza soka tofauti na vijana wanaochipukia akina Ninja, Dante na wengineo na si kwamba sina uwezo wa kucheza.


“Mimi ni kiongozi wa wachezaji wenzangu kwa kuwaelewesha kwani tunahitaji kuhakikisha tunakuwa vizuri kwenye ligi,” alisema Cannavaro.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic