September 1, 2017



Kocha Msaidizi wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja, amefichua siri kuwa watahakikisha wanaibuka na ushindi mkubwa katika mchezo wao dhidi ya Azam FC kama walivyofanya katika mchezo uliopita dhidi ya Ruvu Shooting.

Simba iliibuka na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara msimu huu kabla ya kucheza na Azam FC katika mchezo utakaopigwa Septemba 6, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar.

Mayanja alisema tayari wameshapata dawa ya kufunga mabao ya kutosha bila ya kupiga mashuti ya mbali kama walivyofanya katika mchezo uliopita, hivyo wapinzani wao wanapaswa kujipanga vizuri.

“Baada ya kugundua hatuwezi kupata ushindi mnono kwenye mechi zetu, tukaanza kufanya mazoezi ya kufunga kwa mashuti ya mbali pamoja na kufunga ndani ya boksi.


“Lakini tumeona njia ya kufunga mabao ndani ya 18 kwa mipira ya mwisho imetusaidia kuvuna mabao mengi kwenye mechi moja sasa kitu ambacho tutaendelea kukisisitiza kwa wachezaji wetu katika mechi ijayo dhidi ya Azam tufunge mabao ya kutosha  ili kujiwekee mazingira salama zaidi,” alisema Mayanja.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic