September 1, 2017




Wadhamini wakuu wa ligi ya kikapu ya RBA, Kampuni ya StarMedia Tanzania Limited, sasa wameleta mechi ya All Star ambayo itashirikisha wachezaji vinara katika ligi hiyo. Mechi ya All Star inatarajiwa kuchezwa kesho Jumamosi.

Baada ya kuanza kwa hatua ya robo fainali (playoffs), wapenzi wa mpira wa kikapu watapata nafasi ya kushuhudia wachezaji vinara wa ligi hiyo wakiwapatia burudani stahiki kupitia mchezo wa All Star.

Mchezo utahusisha timu mbili ambazo zimepewa majina ya Nyota na Mambo, majina ya vifurushi vya gharama nafuu vya StarTimes, ndizo zitashuka dimbani katika Uwanja wa Ndani wa Taifa.

Mchezo unatarajiwa kupigwa kati ya saa 2 hadi saa 4 usiku, lakini kabla ya mchezo kuanza kutakuwa na michezo kadhaa ya utangulizi na onyesho kutoka kwa msanii Jay Mo.

Mchezo wa All Star ni sehemu ya ufunguzi kwa hatua ya mtoano ambayo itahusisha timu nane, ili kumpata mshindi na timu tatu zitakazopata nafasi ya kushiriki ligi ya taifa baadaye mwaka huu. Hatua hiyo inatarajiwa kuanza Septemba 6.

Meneja Mahusiano wa Kampuni ya StarTimes, Juma Suluhu, amesema kampuni hiyo itaendelea kusaidia ukuaji wa michezo nchini ikiwa ni sehemu ya uhusiano mzuri kati ya kampuni hiyo na Watanzania.

Ligi ya StarTimes RBA inaonyeshwa mubashara kila siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kupitia Chaneli ya Sibuka Maisha ambayo inapatikana katika king’amuzi cha StarTimes, kwa gharama ya Sh 3,000 kwa mwezi.

Mbali na ligi ya RBA StarTimes ndiyo kampuni yenye kibali cha kuonyesha michuano ya Mpira wa Kikapu Kimataifa (FIBA), na sasa wanaendelea kuonyesha ligi ya kikapu kwa wanawake AfroBasket inayochezwa nchini Mali

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic