October 19, 2017Kocha Juma Masoud ambaye ni mrithi wa Jackson Mayanja yuko jijini Dar es Salaam.

Masoud ametua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) tayari kujiunga na Simba.

Raia huyo wa Burundi anachukua nafasi ya Mayanja ambaye imeelezwa ana matatizo ya kifamilia.

Kocha huyo ameonekana JNIA akisubiri mizigo muda mchache baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam akitokea Kigali.

Masoud amewahi kuwa mmoja wa wachezaji tegemeo wa kikosi cha APR ambacho alicheza kwa mafanikio makubwa.

Kocha huyo anajulikana kwa tabia yake ya ukali pia ni mtu asiyependa mzaha kazini.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV