October 4, 2017


Baada ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pius Buswita, kumalizana na Simba, kisha akapewa nafasi ya kuichezea klabu hiyo akiwa sambamba na pacha wake Thabani Kamusoko katika mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar Jumamosi iliyopita, ametoa ahadi ya kupambana kulitetea kombe lao.

Buswita alikosa michezo minne ya Ligi Kuu Bara kufuatia kufungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), baada ya kubainika kusaini mikataba miwili katika usajili wake jambo lililosababisha akae nje kwa sharti la kurejesha kiasi cha shilingi milioni 10 alizopewa Simba.


Buswita amesema anamshukuru sana Mungu kwa kumwezesha kumaliza tatizo hilo ambalo lilikuwa likimnyima raha tangu lilipotokea na kwamba amefurahishwa na kocha wao Mzambia George Lwandamina kwa kumwamini na kumpa nafasi ya kucheza dakika zote za mchezo wake wa kwanza sambamba na viungo wenzake kama Kamusoko na Raphael Daudi.

“Sina neno zaidi ya kumshukuru Mungu kwa kuniweka huru hivyo ninachoweza kuwaambia wana Yanga kwa sasa ni kuwa nitapambana na wenzangu kadiri Mungu atakavyotujalia ili tuweze kutetea kombe letu maana tupo Yanga kwa ajili ya kuhakikisha tunaitumikia ipasavyo ili mwisho wa ligi tuweze kutwaa kombe.

“Hakuna lugha nzuri ninayoweza kuitumia hapa zaidi ya kuwataka wanachama na mashabiki wetu waendelee kuniamini na kutusapoti kwa ujumla ili nasi tufanye kazi yetu bila kukatishwa tamaa, mbali na hilo pia niwashukuru wachezaji wenzangu na benchi lote la ufundi kwa kunivumilia kipindi chote cha matatizo yangu hivyo nitapambana zaidi ili kulipa muda wao,” alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic