October 30, 2017



NA SALEH ALLY
MECHI ya watani wa jadi, Yanga na Simba haijawahi kwenda kimyakimya, yaani baada ya mechi watu wamalize siku hiyohiyo na kuendelea na mengine.

Hata baada ya siku mbili, tatu au nne, bado mjadala huendelea kuwa motomoto kwa kuwa unahusisha furaha na maumivu katika makundi karibu yote ya wadau wa soka.

Waandishi wangependa kuzungumzia mechi hiyo na inakuwa rahisi kupishana kulingana na mtazamo wa kila mtu katika jambo moja au tofauti.

Lakini kwa mashabiki nao, ikiwezekana kwa matakwa binafsi kwa kuwa hapa kunakuwa hakuna tena taaluma, kila mmoja anaweza kueleza kivyake.

Ubaya au raha zaidi, dunia inabadilika kwa kasi na kila mmoja anaweza kuanika anachoamini kulingana na hamu ya moyo wake na baada ya hapo akaeleza kuwa ni mchambuzi.

Uchambuzi wa jambo kama ni wa kitaalamu ni vizuri pia kuangalia miiko badala ya ushabiki kama ambavyo umeona mashabiki wengi wa Simba wameumia kwa kuwa waliingia uwanjani wakiwa na matokeo yao mfukoni.

Ukiachana na hayo, zaidi nilitaka kulenga mjadala ambao kwangu niliuona unazungumzwa lakini wengi wanaojadili hawakuwa wameangalia jambo la msingi na vizuri kujifunza kupitia kilichotokea kabla hakijayayuka.

Baada ya sare ya watani Yanga na Simba ambao wamemaliza kwa sare ya bao 1-1, wengi wamekuwa wakisema Yanga imetoka sare huku ikiwa na wachezaji wake watatu nyota nje na kama wangekuwepo, ingekuwa ni wakati mgumu kwa Simba.

Kwamba Yanga ilikuwa inawakosa kiungo Thabani Kamusoko na mshambuliaji Donaldo Ngoma raia wa Zambabwe, lakini pia Amissi Tambwe kutoka Burundi. Wengi wanaamini wangekuwepo, ingekuwa ni hatari zaidi.

Ukisikiliza maneno ya mashabiki wengi wakiwemo wale niliowasiliana nao kupitia mtandao wa www.salehjembe.blogspot.com niliona hawakuwa wanaelewa hili na huenda walilizungumza kishabiki sana, kuwasaidia linapaswa kuwa jukumu langu kama sehemu ya wadau.

Nianze na Kamusoko, huenda huyu ungeweza kumuita pengo katika mechi lakini bado si kubwa sana kwa kuwa Yanga imeshinda mechi mbili za Kanda ya Ziwa kwa kuichapa Kagera Sugar kwa mabao 2-1 na baadaye Stand United kwa mabao 4-0 bila ya kuwa na Kamusoko.

Kama unakumbuka katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar kabla ya Yanga kwenda Kanda ya Ziwa, matokeo yalikuwa 0-0 na Kamusoko alikuwemo. Mechi mbili, pointi sita na mabao sita, hakuwemo. Unawezaje kusema angekuwemo dhidi ya Simba ingekuwa hatari zaidi?

Hii inakwenda moja kwa moja kwa Donald Ngoma, naye hakuwemo katika mechi hizo, Yanga ikafunga mabao sita na pointi sita. Vipi ionekane angekuwemo dhidi ya Simba ingekuwa hatari zaidi.

Huenda inaweza kuchekesha zaidi kama Yanga wangesema wanamtegemea zaidi Tambwe kuliko Chirwa ambaye katika mechi tatu sasa mfululizo amefunga mabao matatu akiwa anafunga kila mechi. Alianza dhidi ya Kagera, akafuatia dhidi ya Stand na juzi dhidi ya Simba. Hapa Tambwe na Chirwa nani ni mchezaji wa kutegemewa Yanga kwa sasa?

Kama Ngoma unasema wa kutegemewa, unaweza kumuweka Ajibu nje katika namba 10 kwa sasa kwa kuwa katika mechi tatu amefunga mabao matatu pia, akifunga moja dhidi ya Kagera na mawili dhidi ya Stand, lakini akianzisha kutengeneza bao dhidi ya Simba?

Kuna haja ya kujifunza kwamba, mchezaji tegemeo katika kikosi ni yule aliye fiti. Anayekuwa majeruhi hawezi kuwa tegemeo katika kikosi na kama ni hivyo itakuwa ni kichekesho. 

Hata kwa mashabiki wa Yanga wanaoamini wangekuwa na Tambwe au Ngoma ndiyo wangeshinda wakati wamewahi kuwa nao dhidi ya Simba na hawakushinda.


Vizuri kuwategemea walio fiti na kuamini mchango wao. Epuka kuwakatisha tamaa kwa kuonyesha wao si tegemeo na wangekuwepo wengine wangekuwa zaidi wakati Yanga iliingia uwanjani ikiwategemea wao.

15 COMMENTS:

  1. Nimependa zaidi huu uchambuzi wa Kitaalamu, na ikumbukwe mechi 3/4 zilizopita za Simba na Yanga Tambwe, Ngoma na Thaban walicheza, matokeo yalikuaje? Je alishinda Yanga kwa uwepo wa Tambwe, Thaban na Ngoma?

    ReplyDelete
  2. Nimeuelewa uchambuzi wako, ni vyema kuheshimu mchango wa kila mchezaji anayepangwa, hivi katika msimu wa 2016/2017 , mechi ya kwanza walipotoka 1-1 Ngoma,Tambwe na Kamusoko hawakuwepo? Tena Simba walisawazisha wakiwa pungufu mchezaji mmoja, vipi kuhusu ile ya 2-1 Tambwe na Kamusoko hawakuwepo? Mara hii tena Simba wakiwa pungufu walisawazisha na kuongeza goli la pili, mashabiki tukasema Ngoma angekuwepo Simba isingeshinda, tukumbuke timu inasajili wachezaji wengi ili iwatumie, hivyo kila anayepata nafasi akiitendea haki lazima apongezwe na ndio kaiwakiisha timu yake hvyo.

    ReplyDelete
  3. "Great mind" safi sana kwa kukoleza huu uchambuzi, kila mchezaji ana
    Mchango wake wa pekee na maana sana ktk club, kwahiyo hoja kwamba eti angekuwepo
    Tambwe, Kamusoko na Ngoma haina mashiko kabisa.

    ReplyDelete
  4. Mi nafikiri usiishie kuchambua hayo tu hata baadhi ya meneno ya wasemaji watimu wengine bado hawajakomaa kisoka!msemaji anakwambia viwango vyetu vipi chini lakin ukiangalia hivyo hivyo viwango vya chini tulivyo vya Fifa vimefanya nae amekuwa msemaji wa klabu!Aache dharau viwango bora vinaanzia mpaka wasemaji bora wa klabu!Yatupasa kutafakari.

    ReplyDelete
  5. Hii makala ni ya ajabu na imekaa kishabiki kupitiliza. Nimuulize Saleh ni lini mara ya mwisho Tambwe na Ngoma wamecheza pamoja na Simba ikashinda? Kushinda kwa Yanga kanda ya ziwa bila Kamusoko ndio sababu ya kuona hakuwa muhimu kwa mechi dhidi ya Simba? Ni nani anaweza kubisha kuwa Ngoma, Kamusoko na Tambwe ni wachezaji wa kiwango cha juu kabisa Yanga? Ina maana hata wachezaji wenzao wanajua, kwahiyo uwepo wao tu kama sehemu ya mchezo ni morali tosha hata kama si sehemu ya wale wanaoanza. Hakuna timu duniani isiyoyumba pale key players wanapokuwa hawako fit kucheza. Uandishi lazima uambatane na ueledi, vinginevyo mnaweza kubaki kuwa wasemaji wa vilabu husika

    ReplyDelete
  6. Ndugu Timothy Mkilima msimu wa 2016/2017 hao wachezaji hawakucheza? je Yanga waliifunga Simba? angalia fact usijibu kishabiki

    ReplyDelete
  7. Ndg Timothy uwe mtu wa facts na si kutoa arguments ambazo si documented, misimu tajawa hapo juu wachezaji hao walicheza against Simba na hawakufanya chochote, aidha kuwasifu sana hao Tambwe, Ngoma na Kamusoko ni kuwadharau wachezaji wengine wazalendo wa Club ya Yanga na kusha morali ya hao wachezaji wengine, elewa hili Timothy "no facts no right to comment" facts zinaongea zaidi ya porojo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbaya zaidi walipata matokeo ambayo sio mazuri mbele ya Simba tena timu ya Yanga wakiwa kamili na hao wachezaji "tajwa hapo juu" wakati Simba wakiwa pungufu kwenye mechi zote msimu wa 2016/2017 mimi nadhani tuheshimu kipaji na uwepo wa kila mchezaji anayepata nafasi cha muhimu ni wachezaji wetu kujiamini na kutekeleza majukumu yao ipasavyo.....kumbuka Kamusoko na Ngoma walikuwepo timu ilipohangaika kuwafunga Lipuli fc Uwanja wa Uhuru

      Delete
  8. Yaap! Nadhani ndg. Timothy hana facts zozote zaidi ya porojo zisizo na mashiko.

    ReplyDelete
  9. Tatizo tunachambua mechi kwa kuangalia mechi zilizopita. Kinachotakiwa ni kuangalia nafasi za wazi za kufunga Yanga walizopata Na Simba walizopata...MF nafasi aliyopata Martin kama ingekuwa ni Ngoma au Tambwe ni goli. Kinachotakiwa ni kuwa wachezaji waliokosekana Yanga ni wazoefu.. Pia tofauti Na mechi zilizopita, mechi hii Simba walizidiwa hasa ktk kutengeneza nafasi za kufunga...Sasa kwanini wasijutie kuwa wangekuwepo wakongwe kama Ngoma au Tambwe wasingekosa hata goli moja ktk Nafas zilizopatikana? Salehe Ally acha kudanganya mashabiki, mechi ya juz Simba wangefungwa kama hawavwachezaji wangekuwepo...Ila kwa mechi Simba walizoshinda MF Ile waliokuwa pungufu, Simba walistahili kulingana Na Mpira kiwango kizuri, morali Na pia kutumia nafasi walizopata bila kujali wachezaj kam Tambwe Na Ngoma kucheza. Tunachoaangalia ni mechi ilivyokuwa, nafasi za magoli, aina ya wachezaji kutumia hizo nafasi za magoli. Lkn mechi ya juzi Simba wangefungwa kama Ngoma au Tambwe wangekuwepo kutokana Na uzoefu, pia nafasi za wazivyanga walizopata ukilinganisha Na Simba, Co Salehe Chambua mechi ilivyokuwa, usiwape moyo mashabiki wanaoamini kuwa Simba yao kutokana Na upana wa kikosi walichonacho kuwa ingetakiwa washinde.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Halafu mpira haupo unavyofikiria, hata kama kikosi ni kipana lakini sio kila mechi ni ya kushinda, ni sawasawana Yanga walipocheza na Lipuli FC kila mtu aliamini Yanga watafunga goli nyingi, nini kilitokea? ama Yanga na Mbao FC, inapokutana timu iliyopewa nafasi kubwa na ile inayobezwa basi wachezaji hukaza na kutaka kuwaonyeshea watu sivyo wanavyofikiria, Madrid anafungwa pamoja na upana wa kikosi chake, Man u, Chelsea ....so mpira ni vile unaiendea mechi iliyo mbele yako na si kuangalia matokeo yaliyopita ama laa

      Delete
  10. Tatizo tunachambua mechi kwa kuangalia mechi zilizopita. Kinachotakiwa ni kuangalia nafasi za wazi za kufunga Yanga walizopata Na Simba walizopata...MF nafasi aliyopata Martin kama ingekuwa ni Ngoma au Tambwe ni goli. Kinachotakiwa ni kuwa wachezaji waliokosekana Yanga ni wazoefu.. Pia tofauti Na mechi zilizopita, mechi hii Simba walizidiwa hasa ktk kutengeneza nafasi za kufunga...Sasa kwanini wasijutie kuwa wangekuwepo wakongwe kama Ngoma au Tambwe wasingekosa hata goli moja ktk Nafas zilizopatikana? Salehe Ally acha kudanganya mashabiki, mechi ya juz Simba wangefungwa kama hawavwachezaji wangekuwepo...Ila kwa mechi Simba walizoshinda MF Ile waliokuwa pungufu, Simba walistahili kulingana Na Mpira kiwango kizuri, morali Na pia kutumia nafasi walizopata bila kujali wachezaj kam Tambwe Na Ngoma kucheza. Tunachoaangalia ni mechi ilivyokuwa, nafasi za magoli, aina ya wachezaji kutumia hizo nafasi za magoli. Lkn mechi ya juzi Simba wangefungwa kama Ngoma au Tambwe wangekuwepo kutokana Na uzoefu, pia nafasi za wazivyanga walizopata ukilinganisha Na Simba, Co Salehe Chambua mechi ilivyokuwa, usiwape moyo mashabiki wanaoamini kuwa Simba yao kutokana Na upana wa kikosi walichonacho kuwa ingetakiwa washinde.

    ReplyDelete
    Replies
    1. sasa wewe umejuaje kama nafasi aliyoipata Martin ndo angeipata Ngoma ama Tambwe? kila mtu kaandikiwa bahati yake maishani, ile ilikuwa ni nafasi ya Martin pekee sio ya Tambwe wala Ngoma, huyo Tambwe na Ngoma hawajawahi kukosa magoli wamebaki na kipa? tafuta mechi za msimu uliopita utaelewa hivyo, mechi ya Ndanda ama ile ya Majimaji msimu huu Ngoma alikosa magoli yeye na kipa, ile ya Ndanda kwa kichwa na ile ya Majimaji kwa mguu, ama kule sio kukosa? kukosa kunahesabiwa mechi ya Simba na Yanga tu?

      Delete
  11. Ndg Rama tusiwabeze wachezaji wazalendo, Kocha wa Yanga alisema amewapata mbadala wa Ngoma, Tambwe na Kamusoko, so malalamiko ya angekuwepo Tambwe, Ngoma na Kamusiko hayana ukweli, nadhani kwa sasa viwango cha Ajib, Chirwa na Mashwaiya ni vya kuliko vya Tambwe, Ngoma na Kamusoko, tusiwabeze wachezaji wetu
    Wazalendo bali tuwape moyo na morali, tukubali mechi ilikua ngumu na Simba walikua wamejipanga kuanzia kwa goalkeeper nk.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic