October 30, 2017




Kutokana na sare wanazoendelea kuzipata Simba huenda zikamuondoa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mcameroon, Joseph Omog.

Timu hiyo, ilipata sare yake ya mwisho juzi ilipovaana na Yanga katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katika mechi hiyo, Simba ndiyo ilikuwa timu ya kwanza kupata bao kupitia kwa Shiza Kichuya aliyefunga dakika ya 57 kabla Mzambia, Obrey Chirwa kusawazisha dakika ya 60.

Hivi karibuni zilizuka tetesi za kocha huyo kutimuliwa kutokana na mwenendo mbaya wa matokeo ya mfululizo katika mechi zake za ligi kuu.

Simba hadi hivi sasa imecheza mechi nane za ligi na kati ya hizo imetoa sare mechi nne huku nyingine ikipata ushindi.

Mechi ya kwanza Simba kushinda ni dhidi ya Ruvu Shooting iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru na matokeo kumalizika kwa ushindi wa 7-0 huku Mganda, Emmanuel Okwi akifunga mabao manne pekee.

Mchezo uliofuata walicheza Azam FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Dar ambao ulimalizika kwa suluhu kabla ya kupata ushindi wa mabao 3-0 katika mechi yao ya tatu dhidi ya Mwadui.

Simba walikuja kupata sare nyingine ya mabao 2-2 dhidi ya Mbao FC iliyochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. 
Walipopata sare hiyo, wakaja kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Stand United mchezo uliopigwa Uwanja wa Kambarage, Shinyanga kabla ya kuja kupata sare nyingine ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar.

Baada ya mfululizo huo wa sare, Simba wakaja kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Njombe Mji iliyopanda daraja kwenye msimu huu wa ligi kuu.

Simba juzi Jumamosi waliendelea na mfululizo wa sare walipokutana na Yanga kwenye Uwanja wa Uhuru baada ya kupata sare ya bao 1-1.


Hivyo, basi takwimu zinaonyesha kabisa uwezekano wa timu hiyo kupata ubingwa ni mdogo kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya ya sare wanayoendelea kuyapata katika mechi zao za ligi.

5 COMMENTS:

  1. Yanga0 vs lipuli 0,yanga1, vs njombe 0, yanga1 vs majimaji 1 , yanga 2 kagera 1,yanga 4stand 1

    ReplyDelete
    Replies
    1. hahahahahahaha! mchambuzi mbona hapo sijaelewa, unaposema "mfululizo wa sare" unamaanisha sare zinafuatana, sasa mbona imeonyesha Simba wanashinda mechi 1, inayofuatia wanatoka sare, sasa kwanini usiseme tena "mfululizo wa ushindi?" ninavyofahamu mimi timu zote zenye point 16 ( Simba, Yanga, Azam & Mtibwa Sugar) zote zimeshinda mechi 4, zimetoka sare mechi 4 sasa hapo cha ajabu ni nini?

      Delete
  2. Isitoshe na kushinda kwa Simba ni mabao kibao na ndio wanaoongoza,sasa hao wengine makocha wao hawakuja na mabegi?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic