November 6, 2017



Pamoja na kuendelea vizuri, kikosi cha Azam FC kinaamini kina tatizo la ufungaji na kocha mkuu wa timu hiyo, Aristica Cioaba, raia wa Romania, amesema katika usajili ujao wa dirisha dogo anataka kusajili washambuliaji wawili wazawa.

Azam ambayo juzi Jumamosi iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa katika Uwanja wa Azam Complex jijini Dar, tangu kuanza kwa msimu huu imekuwa na tatizo la ufungaji ambapo kwenye mechi tisa, imefunga mabao saba pekee.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Cioaba alisema kwa muda mrefu amekuwa akihangaika kulitatua tatizo hilo la ufungaji, lakini inaonekana ni sugu, hivyo hana budi kusajili washambuliaji wawili wa maana watakaokata kiu hiyo ya mabao.

“Tunapata ushindi ndiyo, lakini tunafunga mabao machache jambo ambalo halinipendezi. Nimekuwa nikipambana kila siku kuhakikisha tunafunga mabao mengi, lakini naona bado kuna tatizo kwenye ushambuliaji.


“Kutokana na hilo, nitahakikisha kwenye usajili wa dirisha dogo, nasajili washambuliaji wawili wa maana ambao wote ni wazawa, sitachukua kutoka nje ya Tanzania kwa sababu naamini hapa kuna washambuliaji wengi wazuri ambao watanisaidia kutibu hilo tatizo,” alisema Cioaba.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic