November 29, 2017



Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Nassor Cheche, amesema kukosekana kwa kocha mkuu wa timu hiyo, Mromania, Aristica Cioaba katika benchi lao, kwa kiasi fulani inawaathiri wachezaji na kushindwa kupata matokeo mazuri.

Kocha huyo ameyasema hayo juzi Jumatatu baada ya timu yake kuambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar.

Ikumbukwe kuwa, Cioaba amesimamishwa mechi tatu na Bodi ya Ligi kutokana na utovu wa nidhamu ambapo ameanza kuikosa mechi na Mtibwa, kisha ataikosa Stand United na Majimaji.

Cheche alisema: “Ni kweli kukosekana kwake kwa namna moja ama nyingine inawaathiri wachezaji kwani walizoea kumuona akiwa pale na zile hamasa zake zinawafanya wacheze vizuri.

“Hilo limechangia matokeo yetu na Mtibwa kutokuwa mazuri, lakini hali hii nadhani inaweza isiwe endelevu, tutakuwa sawa tu.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic