November 8, 2017




Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imepitia ripoti za michezo yote ya Ligi Kuu Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja Pili (SDL) na kufanya uamuzi ufuatao.

Mechi namba 56 (Stand United 0 v Yanga 4). 
Klabu ya Stand United imetozwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kutokana na golikipa wao kuvaa jezi yenye namba tofauti na ile iliyosajiliwa, kitendo ambacho ni ukiukaji wa Kanuni ya 60(11) ya Ligi Kuu kuhusu Usajili. Adhabu dhidi yao imezingatia Kanuni ya 60(12) ya Ligi Kuu.

Mechi namba 57 (Azam FC 1 v Mbeya City 0). 
Mwamuzi Shakaile Ole Yanga Lai amefungiwa miezi mitatu kwa kutoripoti na kuchukua hatua dhidi ya kitendo cha Kipa Owen Chaima wa Mbeya City kumpiga kofi mshambuliaji wa Azam FC. Kitendo cha Mwamuzi huyo ni ukiukaji wa Kanuni ya 38(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi wakati adhabu dhidi yake imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 38(5) ya Ligi Kuu.

Naye Kamishna wa mechi hiyo, David Lugenge amefungiwa miezi mitatu kwa kushindwa kuripoti tukio hilo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 39 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Kamishna.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic