November 8, 2017


BAADHI YA MASHABIKI WA YANGA AMBAO HAWAKUHUSIKA NA VURUGU HIZO.

Kwa timu ambazo mashabiki wake wamekuwa wakorofi zinatakiwa kuwaambia mapema kwa kuwa zama hizi hakuna utani.
Kwani Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imepitia ripoti za michezo yote ya Ligi Kuu Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja Pili (SDL) na kufanya uamuzi ufuatao.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga nao wamekutana na rungu kutokana na utovu wa nidhamu uliofanywa na mashabiki wake katika mechi namba 58 dhidi ya Simba.


Klabu ya Yanga imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na mashabiki wake kurusha uwanjani chupa zinazosadikiwa kuwa na mikojo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 42(1) kuhusu Udhibiti wa Klabu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic