November 18, 2017


MPIRA UMEKWISHAAAAA


SUB -Hamisi Maingo anaingia kuchukua nafasi ya Kimenya

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 90 Prisons wanaonekana kutokata tamaa, wanaendelea kupambana kupata bao la kusawazisha
Dk 89 Kipa Prisons analazimika kutoka na kuokoa mbele ya Bocco
Dk 87 Manula yuko chini pale, inaonekana amegongana na Mwasote
Dk 86, Kimenya anaachia mkwaju mzuri hapa inakuwa goal kick
GOOOOOOOOOOOOOO Dk 84 Bocco alikuwa kama anaanguka, anageuka na kupiga shuti kali kabisa na kuandika bao 
Dk 81, Mkude anaamua kuacha kutoa pasi, anajaribu mkwaju mkali kabisa, goal kick
Dk 79 kipa wa Prisons anafanya kazi nzuri kuokoa mpira wa kona wa Kichuya, unakuwa wa kurushwa
Dk 78, Simba wanapata kona nyingine baada ya kupiga presha lango la Prisons
SUB Dk 78, Ally Shomari anaingia kuchukua nafasi ya Muzamiru Yassin
Dk 77 krosi nzuri ndani ya lango la Prisons lakini Bocco na Mavugo wanaukosa mpira


Dk 75, Prisons wanapata kona yao ya tatu baada ya Kotei kugongeshwa lakini Sabianka, anapiga kona dhaifu
Dk 74 mpira wa adhabu wa Erasto Nyoni, unatoka juu kidogo ya lango la Prisons, goal kick
Dk 72, Prisons wanamuweka chini Mo Ibrahim
Dk 71 Eliuta anaingia vizuri lakini Kotei anakaa imara na kuokoa vizuri kabisa
Dk 70, Ismail, anafanya kazi ya ziada hapa kuokoa krosi nzuri ya Bocco
KADI Dk 68 Lambart Sabianka wa Prisons analambwa kadi ya njano kwa undava
SUB Dk 67, Laudit Mavugo anaingia kuchukua nafasi ya Kazimoto


Dk 66 Bocco anaruka kupiga kichwa krosi ya Mo Ibrahim, goal kick
Dk 64 Kichuya anaingia na kuachia shuti pasi ya Bocco, Chona analala na kuokoa vizuri kabisa
SUB Dk 60 Niyonzima anakwenda benchi, nafasi yake inachukuliwa na Mohamed Ibrahim
Dk 60 krosi nzuri ya Niyonzima, Prisons wanaokoa vizuri kabisa
Dk 58 Kotei wa Simba yuko chini hapa, aligongana na mchezaji mmoja wa Prisons
Dk 55 Prisons wanafanya shambulizi kubwa zaidi, Simba wanaokoa na kuwa kona, inachongwa na Kimenya, Simba wanaokoa


Dk 52, Manula analazimika kutoka nje ya lango lake na kuokoa, unakuwa wa kurushwa
Dk 48, Kichuya anajaribu akiwa nje ya 18 likiwa shuti lake la kwanza, goal kick
Dk 47 mpira mzuri wa Niyonzima, Bocco anaingia lakini Chona yuko vizuri, goal kick
Dk 45, Prisons wameanza kwa kasi wakionekana wamepania kupata bao la mapema

MAPUMZIKO
-Eliuta anamtoka Kotei anakwenda chini, anaachia mkwaju lakini kipa Manula anadaka vizuri kabisa


DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 44, Kimenya anamkanyaga Kotei hapa, mwamuzi anamuonyesha wakati wachezaji wa Simba wakilalamika
Dk 42, mpira unaendelea kubaki eneo la katikati mwa uwanja kwa dakika tatu sasa
Dk 39 mpira umesimama kuna mchezaji wa Prisons yuko chini pale


Dk 38 sasa, mpira unaonekana kubaki katikati ya uwanja zaidi
Dk 35 Bocco anamchambua Kimenya na kuachia mkwaju mkali kabisa, goal kick
Dk 33, Simba wanapoteza nafasi nzuri kabisa wakiwa wamebaki na kipa wa Prisons, inaokolewa
Dk 30 sasa, kila timu inaonekana kujilinda zaidi na kufanya mashambukizi ya kushitukizaDk 27,krosi ya Niyonzima, Bocco anaweka ndani lakini Mpalile anaokoa mpira ukiwa unavuka mstari
Dk 25, Mlipili anafanya kazi ya ziada kuokoa krosi ya Kimenya na kuwa kona, inachongwa vizuri, Simba wanaokoa
Dk 23, Simba wanagongeana vizuri lakini Kazimoto anachelewa na mwamuzi anasema ni goal kick


Dk 21, Rashid anaingia vizuri lakini mwamuzi anapuliza kipyenga, anasema amefanya madhambi kwa kumsukuma Kotei
Dk 18 Kassim wa Prisons naye anajaribu vizuri kwa kuachia shuti, goal kick
Dk 16, Bocco anawaacha mabeki wa Prisons lakini shuti lake nyanya kabisa
Dk 13, pasi nzuri ya Bocco, Kazimoto anaachia shuti kali kabisa, goal kick
Dk 10, Kichuya anaachia mkwaju mkali kabisa naye hakulenga lango
Dk 7, Mohamed Rashid anaingia vizuri lakini shuti lake halikulenga lango
Dk 1, Prisons ndiyo wanaanza kwa kasi lakini wanaonekana hawako mapema

KIKOSI CHA SIMBA:
Aishi Manula
Erasto Nyoni
Mohamed Hussen "Tshabalala"
James Kotei
Yusuph Mlipili
Jonas Mkude
Shiza Kichuya
Mzamiru Yassin
John Bocco
Mwinyi Kazimoto
Haruna Niyonzima

Sub;
Emanuel  Mseja
Ally shomary
Nicholas Gyan
Laudit Mavugo
Juma Liuzio 
Mohamed Ibrahim "MO"

Jamal Mnyate

1 COMMENTS:

  1. Ni vizuri pia kufahamu kikosi cha wenyeji.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic