KIUNGO mshambuliaji wa kikosi cha Kagera Sugar, Awesu Awesu leo anatarajiwa kuanza kwenye kikosi kitakachomenyana na Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa leo majira ya saa 9:00 alasiri.
Kiungo huyo alionyesha uwezo mkubwa kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali uliochezwa Uwanja wa Taifa, Juni 30 ambapo alifunga bao kwa upande wa Kagera Sugar.
Yanga ilitinga hatua ya nusu fainali baada ya kushinda mabao 2-1 wanatarajia kukutana na Simba, Uwanja wa Taifa, Julai 12.
Hakuweza kumaliza dakika 90 baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano jambo lililopelekea kuonyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi wa kati Shomari Lawi.
Alikosa mchezo mmoja dhidi ya Ligi Kuu Bara Uwanja wa Kaitaba wakati Ruvu Shooting ikikubali kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na Kagera Sugar hivyo leo anaweza kuonyesha makeke.
Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa vijana wake watatoa burudani kwenye mchezo wa leo.
0 COMMENTS:
Post a Comment