November 8, 2017



Mashabiki mbalimbali wa soka na wasomaji wa blog ya SALEHJEMBE wamemuombea nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta apone haraka na kurejea kazini.

Mashabiki hao kupitia blog ya SALEHJEMBE wametuma maoni yao wakimuombea Samatta ambaye ameumia goti apone haraka.

Pamoja na kupitia blog ya SALEHJEMBE, wasomaji hao wa michezo wametuma salamu zao za pole kwa Samatta kupitia mtandao wa Facebook na Instagram kumuombea Samatta ahueni na kupona haraka.

Hali hiyo imetokana na blog ya SALEHJEMBE kuwa ya kwanza kuripoti kuhusiana na suala la Samatta kuumia. Lakini ikawa ya kwanza kueleza kwamba atakaa nje kwa wiki sita akitibiwa baada ya kuumia goti wakati akiitumikia KRC Genk ya Ubelgiji.

Katika kumuombea, wengi wameeleza wanaamini Samatta ni nembo ya Tanzania na kupata kwake mafanikio ni sawa na kuwauza au kuwatangaza wachezaji wengine wa Tanzania.

Hivyo inapendeza akirejea uwanjani mapema na kuendelea kucheza.

Lakini wako waliosisitiza umuhimu wake katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars na wako waliosisitiza anapokuwepo, Stars inapanda kimvuto kuliko anapokosekana.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic