December 4, 2017



Beki wa kulia wa Simba, Shomary Kapombe, wiki hii anatarajiwa kurejea nchini baada ya kwenda India kutibiwa majeraha yanayomsumbua tangu ajiunge na timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu.

Kapombe ambaye aliumia nyonga akiwa na timu ya taifa ya Tanzania ilipocheza dhidi ya Rwanda, Julai, mwaka huu ikiwa ni mechi ya kwanza ya kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (Chan), tangu wakati huo ameshindwa kurudi uwanjani kuitumikia timu yake hiyo mpya.

Mtu wa karibu na Kapombe, amesema kuwa, beki huyo aliondoka nchini wiki mbili zilizopita na kwenda India kutibiwa ambapo jana Jumapili alitarajiwa kupokea ripoti ya daktari anayemtibu, kabla ya kuanza safari ya kurejea nchini kuungana na timu yake.

“Kapombe yupo India anatibiwa ambapo alienda huko kama wiki mbili zilizopita, tayari ameshafanyiwa matibabu na leo (jana Jumapili) anatarajia kukutana na daktari wake ili kumpa ripoti ya maendeleo ya majeraha yake.

“Baada ya hapo ataanza safari ya kurejea nchini ambapo anaweza kufika siku yoyote kuanzia kesho Jumatatu (leo), kama majibu yataonyesha hana tatizo kubwa, basi mara moja ataanza mazoezi kabla ya kurejea rasmi uwanjani,” alisema mtu huyo.


Alipotafutwa Daktari wa Simba, Yassin Gembe, ili aweze kuzungumzia juu ya maendeleo ya Kapombe, hakuwa tayari kusema chochote.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic