December 4, 2017



Jamal Kisongo ambaye ni meneja wa straika, Thomas Ulimwengu, yupo kwenye mchakato wa kuvunja mkataba wa mteja wake huyo dhidi ya timu ya AFC Eskilstuna iliyokuwa ikishiriki Ligi Kuu ya Sweden kufuatia kushuka daraja.

Timu hiyo ndiyo inayojiandaa kumchukua Said Ndemla ambaye amefuzu majaribio akitokea klabu ya Simba ya nchini.

Ulimwengu alijiunga na timu hiyo msimu uliopita ambapo alisaini mkataba wa miaka mitatu na hadi anafikia uamuzi huu hakuwahi kucheza mechi yoyote ya ligi kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya goti anayouguza mpaka sasa.

Kisongo alisema kuwa kwa sasa yupo kwenye mchakato wa kumtafutia timu nyingine Ulimwengu ambapo anaamini mpaka Januari, mwakani, atakuwa amepata timu kubwa inayoshiriki ligi kuu na hatarejea Sweden tena.

Meneja huyo aliongeza kuwa kwa sasa Ulimwengu yupo nchini hapa akifanya mazoezi binafsi ya kujiimarisha baada ya kutoka Ubelgiji alikokuwa kwa mapumziko binafsi.

“Nipo kwenye mchakato wa kumtafutia timu Ulimwengu na ninaamini hadi kufika Januari nitakuwa nimepata ile ambayo inashiriki ligi kuu na hatarudi tena Sweden. Tunataka kuvunja mkataba na wale AFC Eskilstuna kwa kuwa imeshuka daraja licha ya kuwa tumebakiza miaka mawili kwenye mkataba,” alisema Kisongo.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic