December 3, 2017


FULL TIMEDk ya 90 + 3: Mchezo umemalizika, matokeo ni 0-0.
Dk ya 90: Zinaongezwa dakika tatu za nyongeza.
Dk 82: Ametoka Elius Maguri, anaingia Daniel Lyanga.
Dk ya 76: Mbaraka Yusuph anatoka upande wa Stars, anaingia Yahaya Zaid.
Dk ya 67: Kili Stars wanafanya mabadiliko, Hamis Abdallah wa Stars anatoka anaingia Jonas Mkude.
Dk ya 60: Timu zote zinashambuliana kwa zamu.
Dk ya 48: Mchezo umeanza kwa kasi ya taratibu.

Kipindi cha pili kimeanza.

Mapumziko

Dk ya 45: Mwamuzi anapuliza filimbi kukamilisha kipindi cha kwanza.
Dk ya 40: Ajibu anapoteza mpira, Libya wanatumia afasi hiyo kufanya shambulizi kali. 
Dk ya 35: Gooooooo hapana, mwamuzi anakataa, anasema mfungaji wa Libya alikuwa ameotea.
Dk ya 32: Shambulizi kali langoni mwa Libya lakini mashuti mawili yanazuiliwa.
Dk ya 27: Elius Maguri anapata pasi kutoka kwa Gadiel Michael.
Dk ya 24: Kasi imepungua, ni kama timu zinasomana taratibu.
Dk ya 20: Mbaraka Yusuph wa Stars anashambulia lango al Libya inakuwa kona. 
Dk ya 15: Libya wanafika langoni mwa Stars lakini kipa Aishi Manula anafanya kazi nzuri. 
Dk ya 10: Timu zote zinashambuliana kwa zamu.
Dk ya 5: Kili Stars wanafika langoni mara kadhaa lakini wanakosa umakini.
Dk ya 1: Kasi imeanza kuwa kubwa.
Mchezo umeanza.
Timu zimeingia uwanjani, zinapigwa nyimbo za taifa.
Huu ni mchezo wa Kombe la Chalenji ni Kundi A.
Timu ya Taifa ya Tanzania Bara ipo uwanja leo Jumapili Desemba 3, 2017 inacheza dhidi ya Libya katika mchezo wa pili wa michuano ya kuwania Kombe la CECAFA - linaloandaliwa na Baraza la Soka la Afrika Mashariki.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic