December 3, 2017




Kampuni ya kubashiri matokeo ya SportPesa Tanzania, jana imeikabidhi serikali Uwanja wa Taifa wa jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo la kihistoria lilifanyika jana kwenye uwanja huo lililoenda sambamba na ufunguzi wa mashindano ya bunge la Afrika Mashariki wa Kati.

Akikabidhi uwanja huo, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Abbas Tarimba alisema wamekabidhi uwanja huo baada ya ukarabati kumalizika na tayari kwa matumizi.

Tarimba alisema, ukarabati huo umetumia zaidi ya shilingi bilioni 1.4 kwenye sehemu ya uwanja ikiwemo upandaji wa nyasi na udongo.



“Nina furaha ya dhati kusimama mbele yenu kama mwakilishi wa kampuni ya SportPesa na leo (jana) hii katika tukio la kihistoria katika tasnia ya soka nchini la kukabidhi uwanja wa Taifa kwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, hakika ni siku ya kukumbukwa.

“Ukarabati huo uliochukua miezi mitatu katika utengenezaji wa ‘pitch’ kwa maana ya kuotesha uwanja na kuzikuza hadi kufikia hapa.

“Uwanja huu baada ya ukarabati utakaa miaka kumi bila ya kuzikarabati, hivyo utaona ni jinsi gani uwanja huo tumeukarabati kwa kiwanmgo cha juu,” alisema Tarimba.

Kwa upande wa serikali, Waziri wa Habari Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk Harrison Mwakyembe yeye alisema kuwa “Niseme kuwa serikali imeridhika kwa kiwango cha juu cha ukarabati wa uwanja huu wa taifa.



“Niwapongeze na kuwashukuru SportPesa kwa kuomba kujitolea kukarabati uwanja huu, ni jambo jema kwetu, uukarabati huu utatufanya kuutumia kwa muda wa miaka kumi bila ya ukarabati na nimeukagua uwanja huu kiukweli una viwango vizuri,”alisema Mwakyembe.

1 COMMENTS:

  1. SasaMwakiembe ameukagua yeye nimtaalum kweli?😉🤣

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic