January 5, 2018




Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Saa 72) iliyokutana jana Januari 4, 2018 imejadili mechi mbalimbali za Ligi Kuu (VPL) Daraja la Kwanza (FDL) na Daraja la Pili (SDL).


LIGI DARAJA LA PILI
Mechi namba 18 Kundi B (Africans Sports 1 v Kitayosce 2). Kitayosce imepigwa faini ya sh. 50,000 (elfu hamsini) baada ya kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi (pre-match meeting) ikiwa na maofisa watatu badala ya wanne, hivyo kwenda kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Taratibu za Mchezo.


Adhabu dhidi yao katika mechi hiyo iliyofanyika Desemba 29, 2017 jijini Tanga imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu taratibu za Mchezo.


Mechi namba 16 Kundi C (Mighty Elephant 1 v Green Warriors 3). Kocha wa Green Warriors, Azish Kondo amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) baada ya kuondolewa kwenye mchezo (ordered off) na Mwamuzi kwa kutumia lugha chafu.

Adhabu hiyo dhidi ya Kocha Kondo katika mechi hiyo iliyofanyika Desemba 29, 2017 mjini Songea imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 40(10) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Udhibiti wa Makocha.


Mechi namba 18 Kundi C (Mkamba Rangers 0 v Boma 1). Klabu ya Mkamba Rangers imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kuingia uwanjani (pitch).  Adhabu hiyo katika mechi hiyo iliyochezwa Desemba 29, 2017 ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Udhibiti wa Klabu.


Mechi namba 16 Kundi D (Area C v Nyanza). Timu ya Nyanza FC imeshushwa madaraja mawili na matokeo ya michezo yako yote imefutwa kwa kutofika uwanjani bila kutoa sababu yoyote na kusababisha mechi yao dhidi ya Area C iliyokuwa ichezwe Desemba 29, 2017 mjini Dodoma isifanyike.


Uamuzi huo dhidi ya Nyanza FC umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 28(1) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Kutofika Uwanjani. Pia kwa mujibu wa Kanuni ya 28(2) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Kutofika Uwanjani, imepigwa faini ya sh. 2,000,000 (milioni mbili) ambapo sh. 1,000,000 (milioni moja) itachukuliwa na Bodi ya Ligi, na sh. 1,000,000 (milioni moja) italipwa timu pinzani.


Vilevile Kamati imeiomba Sekretarieti kukiandikia barua Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Manyara (MARFA) ili kujua tatizo la timu hiyo.

MECHI YA MVUVUMWA VS FRIENDS RANGERS

Kamati imeipa Friends Rangers ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya Mvuvumwa kuchezesha wachezaji ambao hawajasajiliwa (non qualified) katika mechi ya Kundi A Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati ya timu hizo iliyochezwa Oktoba 29, 2017. Mvuvumwa ilishinda mechi hiyo mabao 4-1.


Uamuzi huo dhidi ya Mvuvumwa umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(18) na 42(20) za Ligi Daraja la Kwanza. Nayo Friends Rangers imepewa ushindi kwa kuzingatia Kanuni ya 14(37) na ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.  


Vilevile viongozi wa Mvuvumwa waliohusika kughushi leseni zilizotumiwa na wachezaji hao ambao hawakusajiliwa watafikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya TFF kwa ajili ya hatua zaidi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic