January 5, 2018





Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Saa 72) iliyokutana jana Januari 4, 2018 imejadili mechi mbalimbali za Ligi Kuu (VPL) Daraja la Kwanza (FDL) na Daraja la Pili (SDL).

Pamoja na yote, pia limejadili masuala ya waamuzi walioshindwa kufanya kazi zao vizuri au kulalamikiwa na wako waliokutana na rungu.


Waamuzi wote wanne wa mechi kati ya Dodoma FC na Alliance; Andrew Shamba, Abdallah Mkomwa, Athuman Athuman na Omari Juma wamefungiwa miaka mitatu kila mmoja kwa kuchezesha mechi hiyo chini ya kiwango. Adhabu dhidi ya waamuzi hao imezingatia Kanuni ya 38(1a) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.

Pia Kamishna wa mechi hiyo Mackshem T. Nzunda amefungiwa miaka mitatu kwa kushindwa kutoa taarifa ya mchezo kwa usahihi. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 39(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Kamishna.


Kamati imeomba suala la waamuzi hao ambao baadhi yao ni wa Ligi Kuu, kupitia TFF liwasilishwe kwenye chombo chenye dhamana ya kisheria ya rushwa kufanyiwa uchunguzi zaidi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic