January 30, 2018



Unaweza ukawa unazungumzia yale mabao mawili ya Yanga na wafungaji wake. Lakini kitaalamu, Azam FC wanaona tofauti kabisa.

Kocha Msaidizi wa Azam, Idd Cheche, amesema kuwa kiungo wa Yanga, Rafael Daud ndiye mchezaji aliyesababisha wapoteze mchezo wao huo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, uliopo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

“Kila tulipokuwa tukifanya mashambulizi ya kasi langoni mwa Yanga na wakifanikiwa kuupata mpira na ukifika miguuni mwa mchezaji huyo, kila kitu kinabadilika, hakuwa na papara na alijitahidi sana kuituliza timu yake.

“Kwa hiyo huyo ndiye aliyekuwa adui yetu mkubwa, lakini tunakubali matokeo na hivyo ndivyo soka lilivyo, tunajipanga kwa ajili ya mechi zetu zijazo,” alisema Cheche.

Ushindi wa Yanga katika mechi hiyo ulikuwa ni mabao 2-1.  Obrey Chirwa raia wa Zambia akifunga la kwanza na  Gadiel Michael akamaliza kazi kwa mkwaju wa Mita 25 baada ya Azam FC kuwa imetangulia kwa bao la Iddi Chilunda mapema katika dakika ya 3.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic