February 25, 2018


George Mganga

Azam FC imesonga mbele katika mashindano ya kombe la FA baada ya kuifunga KMC FC ya Kinondoni, Dar es Salaam kwa jumla ya mabao 3-1.

Mchezo haukuchua muda mrefu, ambapo katika dakika ya kwanza, Frank Domayo aliiandikia Azam bao la kwanza, na baadaye Mbaraka Yusuph akafunga la pili katika dakika ya 7.

Azam FC wakiwa na njaa ya mabao, dakika ya 26, Yahaya Zayd alifunga bao la 3 na mchezo ukawa na mabao matatu kwa Azam huku KMC wakiwa na sifuri.

KMC walikuja kupata bao la kufutia machozi kwenye dakika ya 43 kupitia Hassan, ambaye aliufanya mchezo uende mpaka dakika 90 matokeo yakiwa 3-1.

Azam sasa imekuwa timu ya 3 kuingia hatua ya robo fainali ya mashindano hayo, kufuatia Njombe Mji na Singida United kufika hatua hiyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic