BARCELONA YAICHAKAZA VIKALI GIRONA, SUAREZ APIGA HAT-TRICK
Barcelona imeendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa La Liga baada ya kuicharaza Girona kwa mabao 6-1 huku Luis Suarez akipiga hat-trick.
Wafungaji wa mabao mengine katika mchezo huo ni Leo Messi aliyefunga mawili, pamoja na Philippe Coutinho aliyefunga bao moja na kufikisha magoli mawili akiwa na timu hiyo.
Sasa Barcelona imefikisha jumla ya alama 65 na ikiwaacha mbali mahasimu wao walio nafasi ya 3, Real Madrid ambao wana pointi 51.
0 COMMENTS:
Post a Comment