Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amesema kamwe hawana mpango wa kuishangilia Simba.
Kauli yake inakuwa ni kama kumjibu Msemaji wa Simba, Haji Manara ambaye aliomba Yanga isizomewe kesho pale Uwanja wa Taifa.
Mkemi amesema watakwenda Uwanja wa Taifa kesho kuishangilia Simba wakivaana na St Louis ya Shelisheli, baada ya hapo, Jumapili Simba wataendelea na maisha yao.
“Sisi hatuna mpango wa kuishangilia Simba, hatuna kabisa. Mashabiki wa Yanga wakaishangilie timu yao.
“Hili suala la kuishangilia Simba kwetu halipo na halituhusu. Lakini nawaomba Wanayanga wajitokeze kwa wingi Jumamosi kuishangilia timu yetu,” alisema.
Siku chache zilizopita, Msemaji wa Simba, Haji Manara aliwaomba mashabiki na wanachama wa Simba kutoizomea Yanga Jumamosi kwa kuwa inacheza katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa mwakilishi wa Tanzania.
Kauli hiyo inaonyesha kuwakera baadhi ya mashabiki wako wakimpinga na wengine kumuunga mkono.
Watanzania na hasa mashabiki wa mpira mpuuzeni huyu asiyetaka watanzania kuzishangilia timu zao za Simba na Yanga wakati zikikabiliana na timu za nje. Hilo ndilo siku zote tumekuwa tunashawishi watu kuzipa sapoti timu zetu za ndani punde zinaposhindana na za nje. Jamaa huyu yeye anadhani ni sifa kuwa mkorofi wala sio sifa. Uungwana ni kule kuweka tofauti zetu za ndani na kuwa kitu kimoja pale uwanjani kuzishangilia timu zetu za Tanzania. Jitahidi kuwa kiongozi mwenye mawazo mazuri ya kujenga.
ReplyDeleteNdugu zangu wadau wa Mpira hasa Mpira wa Miguu tutafakari sana kauli za viongozi wetu wa mpira hasa wa tuimu kubwa za Simba na Yanga. Binafsi kama mdau na mpenzi wa mchezo wa Mpira wa Miguu nimeshikwa furaha sana nilipoisikia kauli ya Haji Manara ambaye ni msemaji wa klabu kubwa ya kihistoria nchini Simba sports Club na kwa upande mwingine nimeshikwa na ukakasi mkubwa sana niliposikia kauli ya Salum Mkemi mbaye ni Mjumbe wa kamati tendaji ya klabu kubwa Dar Young africans.
ReplyDeleteNiseme tu kuwa kauli ya Msemaji wa Klubu ya Simba Haji Manara imeonesha kuhitaji mabadiliko chanya yanayoonesha uzalendo wa nchi na halikadhalika inaonesha "this guy has gone to school" Kama kauli hii ya Haji Manara ikafuatwa kadili ya maelezo yake tutakuwa tumefanya jambo kubwa sana katika maendeleo ya Mpira nchini kuliko hata timu ya Taifa kuchukua kombe la AFCON. Nimependa sana mtazamo wake na nilipomsikiliza akisisitiza jambo hili nilitambua kuwa anamaanisha anachokisema.
Kwa upande wa pili Salum Mkemi ambaye ni mjumbe wa Kamati tendaji ya klubu ya Yanga inonesha Umbumbumbu ulioshamili kwa watanzania walio wengi na kuuthibitishia umma kuwa hakustahili kuongoza klabu kubwa kama Yanga.
Mtazamo wangu kama mdau wa mpira ni kuwa Mkemi haifai kuwa Kiongozi wa Yanga na Umma kwa ujumla kwasababu kauli yake inaonesha mgawanyiko katika jamii ileile moja na uchochezi kwa wanafamilia ya mpira nchini. Mkemi huwezi kupata Kiki kwa njia ya kuupotosha umma unaoongoza labda kama hao unaowaita mashabiki wa Yanga nao watakuwa Mambumbumbu kama ulivyo ndipo watakuunga mkono.
Watanzania wenzangu, wadau wa mpira na mashabiki wa Simba na Yanga tuzingatie sana Uzalendo wa nchi ndipo mafanikio ya Mpira yatakuja. Najua wapo watakaonielewa na wapo ambao hawatanilielwa ila tambueni kuwa ili kupata maendeleo katika soka hatuhitaji viongozi kama Salum Mkemi
Nyie wote mnaongea kitu ambacho hamkijui, manara alisema mashabiki wa simba wasiende kuizomea yanga na wala hakusema waende kuishangilia yanga ikicheza. Kwa lugha nyingne waende uwanjan ila wakakae kimya, tafsiri yake ni nini au tofauti yake ni nn na yule aliesema mashabiki wa yanga hawataishangilia simba ikicheza na wadjibout? Au namna lugha zilivyokua presented ndo zimewaacha taabani??.. think big guyz kabla hujatoa povu.
ReplyDeleteSadalla h ndugu yangu hayo yakusema mashabiki wasiende kuzomea na sio kusema waende kushangilia mimi binafsi niliona na kutofautisha. Halihitaji usomi wa PhD au elimu kubwa kutofautisha. Kama unadhani kuwa ni wewe tu umeweza kuona na kutofautisha basi yote ndio hizo kasoro sisi wengine tunazoziona.Ni kweli muungwana hazomei mtu mwenzie hata kama haafikiani naye kwa kutaka kumshangilia. Ni afadhali wende uwanjani ukaangalie bila kumshangilia kuliko KUZOMEA. Kuna tofauti kubwa ya wewe kwa mfano mtu asipokushangilia wakati unafanya jambo zuri na mtu kukuzomea wakati unapambana hufanyi vizuri. Bora Usishangilie lakini Usizomee. Kwenye hili kuthink big? ukubwa gani unaotaka kujikweza nalo hapa. Inahitaji simple minds tu kupambanua hili.
ReplyDelete