February 19, 2018

Mwadui FC

Na George Mganga

Ligi Kuu Soka Tanzania Bara inatarajia kuendelea tena leo kwa viwanja viwili kutimua vumbi.

Mwadui FC ambao katika mechi iliyopita waliizuia Simba kupata alama 3 muhimu, kufuatia goli la dakika za mwisho la kusawazisha kupitia Paul Nonga na kufanya mchezo huo uende sare ya mabao 2-2, leo watakuwa wageni wa Tanzania Prisons.

Mchezo huo ambao utachezwa katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, utaifanya Mwadui ifikishe alama 22 endapo itashinda.

Mpaka sasa Mwadui imecheza michezo 18 sawa na Tanzania Prisons, lakini zikitofautina alama ambapo Prisons ina 26 na Mwadui ina 19.

Mechi nyingine itakayochezwa jioni ya leo ni kati ya Mtibwa Sugar, ambao wataikaribisha Ruvu Shooting katika Uwanja wa Manungu mjini Morogoro.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic