February 19, 2018

Luis Enrique
Huku tetesi zikizidi kueleza kuwa Kocha Antonio Conte anaweza akatupiwa virago muda wowote kutokana na mwenendo wa kikosi chake cha Chelsea kuwa si mzuri msimu huu, taarifa zinasema Luis Enrique anaweza kubeba mikoba yake.


Mbali na uvumi huo wa Enrique kuhitajika Barcelona, kiungo wa FC. Barcelona, Andres Iniesta, amesema kuwa Kocha wake huyo wa zamani ana uwezo wa kushinda mataji katika klabu yoyote duniani.

Iniesta ameeleza kama Enrique ameiwezesha Barcelona kushinda mataji, anaamini hata pale London hilo linawezekana.


"Nadhani anaweza kupata mataji akiwa na klabu yoyote duniani, haiwezi kuwa rahisi sababu Chelsea ni timu kubwa duniani, ila naamini hilo linawezekana. Lakini kama aliweza kuwa mhimili mzuri pale Barcelona, bila shaka hata London itawezekana" - Iniesta.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic