February 19, 2018



Baada ya kuitwanga Mtibwa Sugar kwa mabao 2-1 na kuendelea kubaki katika nafasi ya saba ikwia na pointi 23, Msemaji wa `ruvu Shooting, Masau Bwire amesema wameanzisha mtindo mpya wa Papasa.

Masau amesema mfumo huo utakuwa ni kw akila atakayepita mbele yao, watakachofanya ni “kumpapasa”.

“Nilimuambia ndugu yangu Kifaru (Thobias) kwamba tumekwenda Manungu kuwapapasa. Hakuelewa na kwa kweli alinikaribisha kwa uzuri sana lakini mwisho, tukawapapasa.

“Hii itaendelea kwa kila atakayepita mbele yetu na lengo letu ni kutimiza kile ambacho tuliahidi,” alisema.


Masau aliahidi akihojiwa na kipindi cha Spoti Hausi kinachorushwa na Global Tv Online kwamba watamaliza ligi wakiwa katika nafasi ya tano.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic