February 19, 2018







Kipa Aishi Manula ameumia mazoezini huko nchini Djibouti na imeelezwa ameteguka mkono.

Hali hiyo imezua hofu baada ya mkono wake kufungwa bandeji raini na kulazimika kukaa nje.

Simba inajiandaa kuivaa Gendamarie katika mechi ya Kombe la Shirikisho itakayopigwa kesho.

Tayari Simba ina ushindi wa mabao 4-0 ambao iliupata jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.

Hata hivyo, taarifa kutoka Djibouti zinaeleza kwamba bado haijawa na uhakika kwamba ataukosa mchezo au atacheza na analazimika kusubiri hadi kesho asubuhi kabla ya Kocha Pierre Lechantre hajatangaza kikosi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic