February 20, 2018



Na George Mganga

Baada ya mchezo namba 152 wa Ndanda FC dhidi ya Young Africans kutokuonekana kwenye ratiba ya Ligi, sasa umepangwa katika ratiba na utachezwa February 28 2018.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo, amesema mchezo haukuwa unaonekana kwenye ratiba kutokana na masuala mbalimbali.

Ndimbo amesema mpaka sasa timu zote zimeshapewa taarifa ya kufanyika kwa mchezo huo wa Ligi utakaochezwa katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic