Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kupitia kwa rais wake, Gianni Infantino limekubali michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 17 kufanyika katika mji mmoja wa Dar es Salaam na siyo miji miwili kama ilivyotakiwa awali.
Michuano ya Afcon kwa vijana chini ya miaka 17, inatarajiwa kufanyika nchini mwakani kwa mara ya kwanza kwa Tanzania kuandaa michuano mikubwa kama hiyo.
Akizungumza jijini Dar, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, alisema kuwa amefurahishwa kwa Infantino na ujumbe wake kukubaliana na ombi la kutumia mji mmoja katika michuano ya Afcon jambo ambalo litapunguza gharama na muda.
“Tulimuomba rais aweze kuturuhusu kutumia mji mmoja katika fainali za Afcon tofauti na awali walitaka ichezwe katika miji miwili, tumefurahi wamekubali kwani imepunguza gharama na muda kwani tulikuwa tukihangaika kutafuta mkoa mwingine kuweza kuchezea na tulikuwa tukikutana na changamoto.
“Tumemshukuru kwa kutupa nafasi michuano ya Afcon kuchezwa hapa, tutaitumia vizuri fursa hii,” alisema Mwakyembe.
|
|
|
February 25, 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 COMMENTS:
Post a Comment