February 25, 2018


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ameeleza moja ya makubaliano waliyoyafikia na Rais wa Fifa, Gianni Infantino ni kutengeneza viwanja tisa Tanzania Bara na Visiwani.

Infantino pamoja na Rais wa Caf, Ahmad Ahmad pamoja na ujumbe wa nchi 21 walitua nchini katikati ya wiki hii kujadiliana masuala mbalimbali ya soka ambapo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipata nafasi ya kuzungumza na kiongozi huyo wa soka wa dunia kwa niamba ya Rais John Pombe Magufuli ambaye alikuwa nchini Uganda.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwakyembe alisema kuwa, miongoni mwa mambo waliyojadiliana na Infantino ni ujenzi wa viwanja ikiwa ni moja ya maendeleo ya soka la vijana.

“Rais wa Fifa amekubali ombi letu la ujenzi wa viwanja ambapo ameeleza kuwa kwa ushirikiano wa Fifa, TFF na Serikali kwa pamoja jambo hilo linawezekana kwa kuwa Fifa imeongeza fedha za miradi ya maendeleo kwa nchi za Afrika mara nne ya ile waliyokuwa wakitoa awali, dola za Kimarekani 250,000 ambayo ni sawa na milioni 562,000,000 kwa mwaka, ambayo ilikuwa ikitolewa na rais aliyepita.

“Kwa sasa kiasi ambacho kitatolewa ni dola milioni 1.2ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 2.7, kuanzia hapo tunaweza kuboresha viwanja viwili kila mwaka na iwapo tutasita, Fifa haitasita kuingiza mkono wake.

“Viwanja ambavyo vinatakiwa kutengenezwa ni tisa katika ukanda wa Tanzania Bara na Visiwani ambapo Pemba na Unguja vitatengenezwa viwanja viwili na ukanda wa bara saba.

“Katika maongezi yetu tuliunga mkono na kuipongeza Fifa katika kuendeleza soka la vijana pamoja na kupambana na ubabaishaji na rushwa na kusisitiza kuwa mapambano ndani ya Fifa yanaendelea na kudai kuwa jambo hilo halina mzaha hata kidogo na amesema kupata fedha Fifa ni lazima kuwe na uwazi na uwajibikaji,” alisema Mwakyembe.

Hata hivyo, Mwakyembe aliipongeza TFF kwa kusema kuwa imeanza kufanya kazi kwa kufuata misingi na Fifa tayari wameshaona hilo.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic