Kiungo nyota wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard ameitaka klabu yake hiyo kutafuta kiungo mkabaji “mnyama” ambaye ataisaidia na anaona Mkenya Victor Wanyama anafaa.
Gerrard ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya vijana ya Liverpool, anaamini kikosi chake hicho kinamhitaji Wanyama hasa kwa kuwa kitamkosa Emre Can kwa muda.
Tayari kuna taarifa Liverpool imeanza kulifanyia kazi suala hilo na imeanza kufuatilia nyendo za Wanyama ambaye ni kiungo wa Tottenham.
Hata hivyo, kuna taarifa nyingine hata Chelsea inaonekana inaweza kumtwaa Wanyama kwa kuwa tokea amerejea akitokea katika majeraha, Spurs imekuwa ikimtumia mara chache sana.









0 COMMENTS:
Post a Comment