February 21, 2018



Kocha  Mkuu wa  Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, amefunguka kuwa ni wakati muafaka yeye na kikosi chake kuweza kupambana ili kuhakikisha wanatinga hatua ya nane bora ya Kombe la FA.

Stand United itaikaribisha Dodoma katika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga ambapo mchezo huo unapigwa katika hatua ya 16 Bora ya michuano ya Kombe la FA.

Kocha huyo alisema maandalizi yao ni mazuri na malengo yao makubwa ni kufika katika hatua ya nane bora.

“Malengo ya timu ni kufanya vizuri na kuhakikisha tunasonga mbele na kufika hatua na nane bora, tunajua si michezo rahisi lakini ndiyo nafasi yetu pekee katika kusaka tiketi ya kucheza michezo ya kimataifa.

“Stand wako vizuri na sisi pia tumejipanga kushinda na kusonga mbele kwenye michuano hiyo na naamini mchezo utakuwa mzuri na vijana wangu wana ari ili kuweza kupambana na kupata matokeo,” alisema Julio.

Ikumbukwe bingwa mtetezi wa michuano hiyo, Simba, aliondolewa hatua ya awali dhidi ya Green Warriors.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic