February 21, 2018



Baada ya kutoonekana kwa kipindi kirefu katika kikosi cha Simba, imebainika kuwa straika wa timu hiyo, Juma Liuzio amekuwa nje kwa muda wote huo kutokana na kupewa ruhusa maalumu na benchi la ufundi la timu hiyo linaloongozwa na Mfaransa, Pierre Lechantre.

Mshambuliaji huyo ameachwa kwenye msafara wa timu hiyo ambao ulienda kucheza na Gendarmerie ya Djibouti katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa jana Jumanne. Straika huyo pia alikosa mechi tano za nyuma za kikosi hicho za ligi kuu.

Liuzio amesema kwamba kutoonekana kwake ndani ya kikosi hicho kwenye mazoezi na mechi kulisababishwa na kuwa na matatizo ya kifamilia ambapo alipewa ruhusu maalumu na makocha wake kwa ajili ya kuyatatua matatizo hayo kabla ya kuungana na wenzake.

“Unajua kwamba sikwenda kule Djibouti na wenzangu kwa sababu nilikuwa na ruhusa maalum kutoka kwa kocha baada ya kupata matatizo ya kifamilia ambapo niliomba nikashughulikie na ndiyo maana sikuonekana uwanjani kwa kipindi kirefu.


“Ila kwa sasa kila kitu kimeshakaa sawa na nitaungana na wenzangu muda mfupi baada ya kurejea kutoka kule Djibouti walipokwenda kwenye mechi ya Shirikisho Afrika,” alisema Liuzio. 

SOURCE: CHAMPIONI

4 COMMENTS:

  1. Kichwa cha habari mbona hakiendani na kilichoandika ndani yake? Waandishi wa kibongo kazi bado ipo tena sana!

    ReplyDelete
  2. Waandishi hawa bomu kabisa, nadhani wanapaswa warudi shule, kichwa cha habari na maelezo haziendani,maelezo hayaonyeshi kuwa Luizio kaomba kuondoka Simba, waandishi mnatutia aibu.

    ReplyDelete
  3. Vilaza hawa sijui shule gani wameenda wanauza habari kwa kushtua kwenye kichwa cha habari ndani ya habari yenyewe tofauti kabisa wanadhani wao wajanja kuliko wengine hii shida tupu

    ReplyDelete
  4. Nawashangaa sana walioandika habari je huyo luzio akikuuliza utasemaje

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic