February 21, 2018



Kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude ameutaka uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuongeza umakini katika hatua ya lala salama ya Ligi Kuu Bara ili kuepukana na vitendo vya hujuma ambavyo vinajitokeza.

Mkude ametamka hayo baada ya kudai kuwa kuna njama ambazo zinafanyika na wapinzani wao katika ligi  kuwaumiza baadhi ya wachezaji wa timu hiyo ili kuwapunguza kasi.

"Binafsi namkubali sana Bocco na anapokosekana katika kikosi chetu huwa sijisikii vizuri kwani ni mmoja kati ya washambuliaji wakuigwa hapa nchini."


“Ni mpambanaji na haogopi kuumia anapokuwa akipambana kuitafutia ushindi timu yetu, lakini kuna mchezo mchafu ambao umeanza kufanyika wa kutaka kumuumiza makusudi ili tu kuipunguza makali timu yetu, hiyo siyo sawa TFF wanatakiwa kuwa makini katika hilo,” alisema Mkude baada ya Bocco kuumizwa katika mechi ya ligi dhidi ya Mwadui FC.

SOURCE: CHAMPIONI

2 COMMENTS:

  1. TFF chukueni hatua kali za makusudi kwa mchezaji anayemuumiza kwa makusudi mchezaji mwingine. Haya yanawatia vilema wenzao kwanini mnawavumilia wachezaji wa aina hiyo? Wafungieni msimu mzima asicheze aende kulima mihogo. TFF lazima ichukizwe na vitendo vya kihuni wanavyofanya wachezaji tena sio wengi wachache tu wasiopenda ustaarabu. Bofu mmojawapo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic