Inaonekana kuwa beki wa kushoto wa Simba, Mohamed Hussein Zimbwe analazimika kukaza buti hasa, la sivyo, First Evelen atakuwa akiisikia tu radioni.
Hii inatokana na beki Mghana, Asante Kwasi ambaye Simba ilimsajili kama beki wa kati kuonyesha uwezo mkubwa akicheza pembeni kushoto.
Kwasi amekuwa chachu ya mabao mengi ya Simba huku akionyesha uwezo mkubwa wakati wa kulinda na kushambulia.
Krosi zake nyingi zimekuwa tegemeo la kusababisha mabao ya Simba au kutengeneza mashambulizi bora.
Hii inamfanya Zimbwe ambaye alikuwa “mwenye namba” msimu uliopita kuwa katika wakati mgumu sana.
Zimbwe ameendelea kubaki benchi na chaguo la kwanza la Kocha Mkuu Mfaransa, Pierre Lechantre na msaidizi wake Mrundi, Masoud Djuma kuwa ni Kwasi na kama ataendelea kuwa fiti basi Zimbwe lazima afanye kazi hasa.







Kabisa kila namba simba inaushindani mkali. Angalia beki ya kati mlipili kama hataki kubanduka tena. Vipi mbonde akiwa fiti. Vipi Juko Murshidi? Hali ya ushindani wa namba katika club ya simba unafanana na changamoto wanazokutana nazo wachezaji wetu wanapojaribu kutafuta ajira nje ya nchi na kuishia kurudi nyumbani lakini sasa kwa vijana waliopo pale simba ile changamoto ya kupata nafasi ya kucheza kama wanamalengo ya kufika mbali basi wasiichukulie kama kero bali waichukulie kama bahati. Hakika kwa vijana wanaochezea simba wanatakiwa kuwa makini kufuata maelekezo ya bench lao la ufundi kwani bench lao la ufundi hivi sasa limekamilika lenye uwezo wa kumjenga mchezaji kwenda kutafuta ajira sehemu yeyote ile na akafanikiwa katika maisha ya soka. Inatokezea wakati katika maisha mtu hutamani kufanya kazi bure kutokana na maslahi makubwa ya ujuzi utakayoyapata kuliko hata mshahara. Lakini sidhani kama vijana wetu wa kitanzania wana mawazo kama hayo.
ReplyDeleteKlabu kama Simba haiwezi kumsajili mchezaji kama hawajiridhisha kwamba anaweza na atakuwa msaada kwao. Sasa mchezaji labda awe na majeruhi lakini mchezaji kukubali kukaa bench kizembe zembe mbele ya kocha mwenye kuangalia uwezo wa mtu sio sura ni aibu na kutojitambua kwa mchezaji. Hakuna uoga wala muhali wa mtu katika kujitengezea heshima kazini ni kupambana tu kuhakikisha unajijengea nafasi yako nakuwa chaguo la kwanza la bosi wako.
ReplyDelete